23.6 C
New York

Burna Boy, Shakira kinawaka tena

Published:

MIAMI, Marekani

MKALI wa Afrobeats, Burna Boy, amekutana kwa mara nyingine na staa wa muziki wa Pop, Shakira, kwa ajili ya shoo yao nyingine msimu huu wa fainali za Kombe la Dunia.

Wanamuziki hao walitumbuiza wakati wa ufunguzi Juni 11, 2026, na sasa watafanya hivyo tena wakati wa mapumziko katika mechi ya fainali itakayochezwa kesho (Julai 19, 2026).

Burna Boy na Shakira wamekutana na kufanya mazoezi katika Uwanja wa MetLife utakaotumika kwa fainali hiyo itakayozikutanisha Argentina na Hispania.

Katika picha aliyoposti katika mtandao wa kijamii wa X, Burna Boy anaonekana akicheka na kupiga stori na mke huyo wa zamani wa mkongwe wa Barcelona, Gerard Pique.

Kupitia shoo hiyo baada ya dakika 45 za kwanza, Burna Boy na Shakira wanatarajiwa kutumbuiza kwa pamoja wimbo wao wa ‘Dai Dai’, ambao ni maalumu kwa ajili ya fainali za mwaka huu.

Related articles

Recent articles