21.8 C
New York

Kane, Alvarez nani kuziba pengo la Lewandowski?

Published:

CATALUNYA, Barcelona

BADO mabosi wa Barcelona wanaumiza vichwa kujua ni straika yupi sahihi kati ya Julian Alvarez wa Atletico Madrid na Harry Kane wa Bayern Munich.

Kwa sasa, Barcelona wanahaha kuziba pengo la straika aliyeondoka kikosini, Robert Lewandowski.

Kane anakaribia kumaliza mkataba wake na Bayern na ameweka wazi kuwa ataijua hatima yake baada ya fainali za Kombe la Dunia zinazoendelea.

Straika huyo raia wa England, ambaye anakaribia kutimiza umri wa miaka 33, ameonesha nia ya kuongeza mkataba utakaombakiza Allianz Arena.

Msimu uliomalizika wa 2025-26, Kane alikuwa moto wa kuotea mbali, ambapo alimaliza na mabao 61 ya michuano mbalimbali.

Alvarez (26), amefunga mabao 49 na kutoa ‘asisti’ 17 katika mechi 106 alizocheza tangu aliposajiliwa na Atletico Madrid akitokea Manchester mwaka 2024.

Katika msimu uliomalizika, 2025-26, alifunga mabao 20 na asisti tisa kwenye michezo 49.

Muargentina huyo anapatikana kwa ada ya Pauni milioni 432 na hivi karibuni alisema anataka kuondoka Atletico Madrid.

“Sidhani kama ni wakati sahihi kuzungumzia hilo lakini sitaki kuficha (nia ya kuondoka),” alisema.

“Nataka kuwa mkweli. Nafikiri jambo zuri kwa kila mchezaji ni usajili. Nataka kutimiza ndoto yangu.”

Related articles

Recent articles