25.3 C
New York

Marekani yajitoa mapambano dhidi ya Ukimwi Afrika Kusini

Published:

WASHINGTON DC, Marekani

SERIKALI ya Marekani imetangaza kusitisha ufadhili wa programu zote za mapambano dhidi ya Ukimwi nchini Afrika Kusini.

Afrika Kusini inaongoza duniani kwa kuwa na waathirika wengi wa ugonjwa huo, wakitajwa kufikia zaidi ya milioni nane.

Hatua hiyo ya Marekani kujitoa ni mwendelezo wa uhusiano mbaya uliopo kati yake na Taifa hilo la Afrika.

Utawala wa Rais Donald Trump umekuwa ukiishutumu Serikali ya Afrika Kusini kwa kile unachodai kuwa imeshindwa kuwalinda watu weupe nchini humo dhidi ya uonevu.

Kwa upande wake, Wizara ya Afya ya Afrika Kusini imeeleza kuwa licha ya kutokupokea taarifa rasmi ya Marekani, tayari imejipanga kujitegemea katika programu zake za kukabiliana na Ukimwi.

Related articles

Recent articles