LAGOS, Nigeria
HIYO ni kauli ya staa wa soko la muziki wa Nigeria, Daniel Benson, maarufu kwa jina la BNXN, baada ya kuwasili akitokea Los Angeles nchini Marekani.
Katika mazungumzo yake kupitia mtandao wa kijamii wa TikTok, BNXN amedai kuwa maisha ya Lagos ni magumu kuliko Marekani.
Aidha, msanii huyo amesema katika maisha yake akiwa Los Angeles, hajawahi kuona ombaomba wa mitaani kama ilivyo Lagos.
“Nilikuwa namwambia mtu, kwamba tangu nikiwa Marekani, sijawahi kuona mtu anakuja kukuomba pesa. Watu wanateseka sana hapa (Nigeria).
“Lagos maisha ni ghali sana kuliko Los Angeles. Ukiacha gharama za nyumba, mambo mengine siyo bei kali ukiwa LA (Los Angeles),” amesema.


