32.2 C
New York

Kiongozi wa upinzani Guinea aendelea kushikiliwa

Published:

BISSAU, Guinea Bissau

MAHAKAMA ya kijeshi ya Guinea Bissau imeagiza kiongozi wa siasa za upinzani nchini humo, Domingos Simoes Pereira, kuendelea kushikiliwa.

Mwanasiasa huyo anayetumikia kifungo cha ndani anakabiliwa na mashitaka ya kusuka mpango wa kuipindua Serikali.

Pereira, kiongozi wa Chama cha African Party for the Independence of Guinea and Cape Verde (PAIGC), alikamatwa baada ya jeshi kumpindua Rai Umaro Sissoco Embalo mwaka 2025.

Baada ya kutolewa gerezani Januari, 2026, alihamishiwa kutumikia kifungo cha ndani akiwa nyumbani kwake.

Katika mashitaka yanayomkabili, Pereira anatajwa kuhusika kwenye majaribio mawili ya kupindua Serikali, moja la mwaka 2023 na jingine la mwaka 2025.

Mmoja ya wanasheria wake, Joao Paulo Indeque, amesema mashitaka dhidi ya mteja wao ni ya kisiasa kwani hakuhusika kwa namna yoyote katika hayo yanayotajwa kuwa ni majaribio ya kuipindua Serikali.

Related articles

Recent articles