23.5 C
New York

PSG yaizima Arsenal, yabeba tena Ligi ya Mabingwa

Published:

BUDAPEST, Hungary

MATAJIRI wa Paris, PSG, wamelitetea taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya baada ya ushindi wa penalti 4-3 dhidi ya Arsenal katika mchezo wa fainali uliochezwa leo Mei 30, 2026 mjini Budapest, Hungary.

Dakika 120 za mtanange huo zilimalizia kwa sare ya bao 1-1, Arsenal wakitangulia kupitia kwa Kai Havertz (Dk. 5), kabla ya PSG kusawazisha kupitia Osumane Dembele (Dk. 64).

Kwa upande mwingine, hiyo imekuwa fainali ya 16 kwa kocha wa PSG, Luis Enrique, kushinda na kubeba taji kati ya 19 alizoingia akiwa na klabu mbalimbali.

Waliokosa mikwaju ya penalti kwa upande wa Arsenal ni Gabriel na Eberechi Eze, huku PSG wakikosa kupitia kwa Mendes.

Waliopiga na kupata kwa upande wa PSG ni Lucas Beraldo, Achraf Hakimi, Desire Doue, Goncalo Ramos, wakati Viktor Gyokeres, Declan Rice na Gabriel Martinelli walipata kwa upande wa Arsenal.

Related articles

Recent articles