21.5 C
New York

Unai Emery aandika historia Ligi ya Europa

Published:

LONDON, Uingereza

KOCHA raia wa Hispania, Unai Emery, ameweka rekodi baada ya kuiongoza Aston Villa kutwaa ubingwa wa Ligi ya Europa kwa ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Freiburg.

Mechi hiyo ya fainali ilichezwa Mei 20, 2026 mjini Istanbul, Uturuki, na Emery anakuwa kocha wa kwanza kutwaa taji la Europa akiwa na timu tatu tofauti.

Kocha huyo wa zamani wa Arsenal, alibeba ‘ndoo’ hiyo mara tatu akiwa na Sevilla, kabla ya kuipa tena mara moja Villarreal, zote za Ligi Kuu ya Hispania (La Liga).

Katika mchezo wao dhidi ya Freiburg ya Bundesliga, Villa walipata mabao yao kupitia kwa Youri Tielemans, Emiliano Buendía na Morgan Rogers.

Kwa upande mwingine, Emery anakuwa kocha wa kwanza katika historia ya Villa kuiongoza timu hiyo kutwaa ubingwa wa Ulaya.

Related articles

Recent articles