25.9 C
New York

Usajili dirisha kubwa Ulaya: Nani aondoke, nani abaki? – MAN UNITED

Published:

MANCHESTER, Uingereza

WALIMALIZA msimu wa 2025-26 wakiwa nafasi ya tatu kwenye msimamo wa Ligi Kuu ya England (EPL) na kukata tiketi ya kwenda Ligi ya Mabingwa Ulaya (2026-27).

Mafanikio hayo yamempa mkataba wa miaka miwili kocha Michael Carrick na sasa analazimika kufanya maboresho ya kikosi ili kujiimarisha zaidi.

Joshua Zirkzee ataondoka, kama ilivyo kwa Casemiro na Tyrell Malacia, ambao wamethibitisha kutimka majira haya ya kiangazi.

Kwa upande mwingine, Rasmus Hojlund ameshakamilisha usajili wa kubaki Napoli baada ya kucheza kwa mkopo klabuni hapo.

Carrick ameshamsajili kiungo wa Atalanta ya Serie A, Ederson, wakati huo pia akihusishwa na viungo Mateus Fernandes (West Ham), Sandro Tonali (Newcastle), Aurelien Tchouameni (Real Madrid), Elliot Anderson (Forest), na Carlos Baleba (Brighton).

Pia, Man United inasaka kipa mpya wa kunisaidia kazi Senne Lammens. Wanahusishwa zaidi na Lewis Hall wa Newcastle.

Aidha, Carrick anahitaji mshambuliaji wa kati wa kumpa changamoto Benjamin Sesko, huku taarifa zikidai kuwa huenda Marcus Rashford akarejeshwa Old Trafford baada ya kumaliza mkopo wake Barcelona.

Related articles

Recent articles