LONDON, Uingereza
KLABU ya Chelsea imeonesha kuvutiwa na mshambuliaji wa zamani wa Liverpool, Darwin Nunez.
Nunez raia wa Uruguay aliondoka Anfield mwaka jana na kutua Al-Hila ya Saudi Arabia baada ya kukosa namba katika kikosi cha kocha Arne Slot.
Hata hivyo, nyota huyo mwenye umri wa miaka 26 amekuwa akihusishwa na mpango wa kuondoka Saudia mwishoni mwa msimu huu.
Taarifa za kuondoka Saudia zilianza baada ya klabu yake hiyo kumsajili straika wa zamani wa Real Madrid, Karim Benzema.
Kwa msimu huu, tayari Nunez ameshaingia kambani mara tisa na kutoa ‘asisti’ tano katika mechi 24 alizoshuka dimbani.


