9.5 C
New York

Mechi hizi hata FIFA haiziruhusu

Published:

LONDON, Uingereza

KWA mara kadhaa, siasa zimefanikiwa kuingia na kuathiri mchezo wa soka. Ni kama ilivyo sasa kwa Urusi na Ukraine. Baada ya Urusi kuivamia Ukraine mwanzoni mwa mwaka 2022, Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA) lilitoa uamuzi wake.

Ni uamuzi wa kuzizuia klabu za Urusi, pamoja na timu ya taifa, kushiriki michuano ya kimataifa.
Urusi ilikata rufaa kupinga uamuzi huo wa FIFA lakini ikabaki hivyo, huku Ukraine ikiruhusiwa kuendelea kushiriki

Kwa mazingira hayo ya uadui, ni ngumu kuona FIFA ikibariki mechi inayoyakutanisha mataifa hao.
Ni kama ambavyo pia FIFA haitaruhusu Ukraine kukutana na Belarus, ambao ni washirika wakubwa wa Urusi.
Mechi nyingine ni kati ya Hispania na Gibraltar.

Mataifa hayo yamekuwa na uhasimu mkubwa wa kisiasa kwa miaka mingi. Wakati wa fainali za EURO za mwaka jana, mastaa wa Hispania, Rodri na Alvaro Morata, waliadhibiwa na Shirikisho la Soka la Ulaya (UEFA) kwa kauli zao za kichokozi dhidi ya Gibraltar.

Kwa upande mwingine, kuna mechi kati ya Armenia na Azerbaijan. Kwa miaka mingi, tangu miaka ya 1990, mataifa hayo yana uadui mkubwa wa kisiasa.

Mwaka 2020, Kamati ya Utendaji ya UEFA iliweka wazi kuwa hakuna mechi ya mashindano itakayochezwa Armenia na Azerbaijan.

Pia, ni ngumu kuona FIFA ikiruhusu mechi kati ya Kosovo na mataifa matatu; Serbia, Urusi na Bosnia‑Herzegovina.

Kosovo ilijitangazia uhuru mwaka 2008 kwa kujitoa kwenye mamlaka ya Serbia. Tangu hapo, uhusiano si mzuri kati ya mataifa hayo.

Vilevile, Kosovo ‘inazichukia’ Urusi na Bosnia kwa sababu mataifa mawili hayo yamegoma kuutambua uhuru huo na sasa yanaiunga mkono Serbia.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img