2.8 C
New York

Jenerali wa jeshi Urusi auawa

Published:

MOSCOW, Urusi

URUSI imepata pigo baada ya Jenerali wake wa jeshi kuuawa katika shambulio la bomu, kwa mujibu wa taarifa ya Serikali ya nchi hiyo.

Taarifa rasmi zinaeleza kuwa gari alilokuwa akiendesha Luteni Jenerali Fanil Sarvaror lilishambuliwa kwa bomu asubuhi ya leo Desemba 22, 2025 akiwa mjini Moscow.

Kwa mujibu wa taarifa, bomu hilo lilitegwa katika gari na Sarvarov mwenye umri wa miaka 56 aliyekuwa kiongozi wa Idara ya mafunzo ya jeshi allmepoteza maisha akiwa hospitali kwa matibabu.

Aidha, kwa mujibu wa kile kilichoelezwa na Serikali ya Urusi, Ukraine inahusika katika tukio hilo la kutega bomu kwenye gari la Sarvarov. Ukraine haijajibu.

Sarvarov anakumbukwa kwa kusimamia operesheni kadhaa za kijeshi, ikiwamo ya hivi karibuni nchini Syria kati ya mwaka 2015-2016.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img