PARIS, Ufaransa
RAIS wa zamani wa Ufaransa, Nicolas Sarkozy, anatatajiwa kufikishwa mahakamani ifikapo mwaka 2027, hatua inayomlenga pia mkewe, Carla Bruni-Sarkozy.
Sarkozy anakabiliwa na mashitaka mengi, kubwa ikiwa ni kutumia fedha alizopewa kinyume cha utaratibu na aliyekuwa Rais wa Libya, Muammar Gaddafi, katika kampeni za urais.
Licha ya kukana mashitaka hayo, taarifa zinaeleza kuwa upo Ushahidi wa kutosha utakaowatia hatiani wanandoa hao.
Tangu alipong’oka madarakani mwaka 2012, Sarkozy amekuwa akikabiliwa na mashitaka mengi ya jinai. Mwaka 2024, alihukumiwa kifungo cha mwaka mmoja, ingawa hukumu hiyo ilipunguzwa hadi miezi sita.
Septemba, 2026, Sarkozy alihukumiwa kifungo cha miaka mitano gerezani na kuwa rais mstaafu wa kwanza wa Ufaransa kwenda rumande, lakini aliachiwa siku 20 baadaye.


