WINDHOEK, Namibia
POLISI nchini Namibia wamekamata gari lililokuwa limebeba mizoga miwili ya ng’ombe yenye thamani ya Dola 16,000 za Namibia [Zaidi ya Shilingi milioni 2.5 za Tanzania].
Gari hilo liliachwa na watu wanaoshukiwa kuwa ni wezi wa mifugo waliotoweka baada ya kubainika katika Kijiji cha Mashare kilichopo Mkoa wa Kavango Mashariki.
Naibu Kamishna wa Polisi, Moses Simaho, amesema tukio hilo lilitokea usiku wa kuamkia Jumapili, Novemba 15, 2026.
Kamishna Simaho ameeleza kuwa vikosi vya ulinzi vinaendelea na uchunguzi mkali, sambamba na kuwasaka watuhumiwa hao waliokimbia.
Ameongeza kuwa uchunguzi huo unafanyika kwa kuzingatia Kifungu cha 2 cha Sheria ya Kuzuia Wizi wa Mifugo Namba 19 ya mwaka 2004, iliyofanyiwa marekebisho, inayohusu kumiliki au kusafirisha mifugo inayoshukiwa kuwa imeibwa.


