WASHINGTON DC, Marekani
RAIS Donald Trump ameipa onyo Iran akisema ataisambaratisha endapo itaendelea na mipango yake ya siri ya kutaka kuishambulia Washington.
Trump, Rais wa 47 wa Marekani, amekuja na ujumbe huo katika mahojiano yake na kituo cha televisheni cha Fox News wakati huu akiwa China kuhudhuria Mkutano unaoendelea.
Katika mahojiano hayo, amesema anaamini Iran ina hasira na Washington baada ya kampeni ya Marekani ya kuizuia kuzalisha silaha za nyuklia.
Aidha, ameyasema hayo zikiwa ni siku chache tu baada ya vyombo vya usalama vya Marekani kudai kuwa Iran inalenga kuwaua viongozi wa Serikali ya Trump.
“Vizuri, kuna viashiria vya Iran kutaka kutumia gesi za sumu na silaha zingine za kibaiolojia kwa sababu tulizuia utengenezaji wa silaha za nyuklia,” amesema na kuongeza: “Ngoja tuone kitakachotokea Januari Mosi [2027] … Kama watafanya hivyo, tutawasambararisha.”
Kwa upande wake, mamlaka za Iran zimeibuka na kukanusha madai kuwa zimepanga kuishambulia Washington au kuua viongozi wa Serikali ya Marekani.


