10.4 C
New York

Hakeem Jeffries aandika historia Spika wa Bunge Marekani

Published:

WASHINGTON DC, Marekani

HAKEEM Jeffries wa Chama cha Democratic ameandika historia ya kuwa mwanasiasa wa kwanza mweusi kuingia kwenye kinyang’anyiro cha kuwania nafasi ya Spika wa Bunge nchini Marekani.

Jeffries [56], ameweka rekodi hiyo baada ya kupata kura 251 katika Uchaguzi wa ndani wa Democratic uliofanyika jana Novemba 18, 2026.

Kwa mujibu wa taarifa iliyoripotiwa na vyombo vya habari vya Marekani, mwanasiasa huyo amekosa kura 11 pekee, hivyo kutangazwa kupeperusha bendera ya Chama chake hicho.

Hivyo, Jeffries anatarajiwa kuwa Spika wa Bunge endapo atathibitishwa na Bunge kupitia kura zitakazopigwa na wawakilishi wote Januari 3, 2027.

Akizungumza baada ya Chama chake kumpitisha, ameahidi kuwa endapo atachaguliwa na Bunge, atasimamia misimamo mikali dhidi ya Serikali ya Rais Donald Trump.

Aidha, Jeffries amesema bila upendeleo wala kuonea, atahakikisha Bunge linasimamia uchunguzi wa kina juu ya madhaifu ya Serikali, hasa shutuma za rushwa.

Related articles

Recent articles