14.5 C
New York

Samsung yaongoza mauzo ya ‘smartphone’ Afrika

Published:

BEIJING, China

KAMPUNI ya teknolojia ya Samsung ya China ndiyo inayoongoza kwa mauzo ya ‘simu-janja’ [smartphones] barani Afrika kufikia hatua hii ya robo ya pili ya mwaka 2026.

Kwa mujibu wa kampuni ya takwimu za masoko ya TechInsights, Samsung iliongoza kwa mapato katika robo ya kwanza, kama ilivyofanya pia kwenye robo ya pili ya mwaka huu uliobakiza miezi isiyozidi miwili kumalizika.

Licha ya mauzo ya ‘smartphone’ kushuka kwa asilimia 16.6 barani Afrika, mauzo ya simu hizo kwa upande wa Samsung yamepanda kwa asilimia 34.8.

Hiyo ni hatua kubwa kwa Samsung katika soko la Afrika kwani mauzo yake yalikuwa asilimia 22.4 mwaka 2024, kisha asilimia 26.5 mwaka 2025.

Kwamba kwa mwaka huu, matarajio ni mauzo yake kufikia asilimia 38.7, sawa na ongezeko la asilimia zaidi ya 16 ndani ya miaka miwili tu.

Simu-janja zimekuwa na soko kubwa Kusini mwa Jangwa la Sahara, ambapo tafiti zinaeleza kuwa kwa mwaka jana pekee, ilifanyika miamala ya fedha yenye thamani ya Dola trilioni 1.4.

Related articles

Recent articles