20.9 C
New York

Waingereza waliowahi ‘kusepa’ na Ballon d’Or

Published:

LONDON, Uingereza

HARRY Kane ameondoka na Ballon d’Or ya mwaka huu [2026] lakini haimaanishi kuwa straika huyo ndiye Muingereza wa kwanza kuiweka mkononi tuzo hiyo maarufu zaidi katika ulimwengu wa soka.

Na badala yake, Kane anayekipiga Ligi Kuu ya Ujerumani akiwa na Bayern Munich, anakuwa Muingereza wa tano kutwaa tuzo hiyo, licha ya kwamba ni wa kwanza baada ya miaka 25 kupita.

Kwa Waingereza, tuzo hiyo ilitua kwao kwa mara ya kwanza mwaka 1956 baada ya Stanley Matthews kutangazwa mshindi. Alinyakua tuzo hiyo akimzidi pointi tatu aliyekuwa staa wa Real Madrid, Alfredo Di Stefano.

Wakati huo, Matthews alikuwa akikipiga Blackpool ya England na alitwaa tuzo akiwa na umri wa miaka 41. Hii ilimpa rekodi ya kuwa mchezaji ‘mzee’ zaidi kutangazwa mshindi wa Ballon d’Or.

Mara ya pili kwa Waingereza kuibeba Ballon d’Or ilikuwa mwaka 1966 kupitia kwa Bobby Charlton, wakati huo akiwa kiungo tegemeo wa klabu ya Manchester United.

Alimpiku kwa pointi chache mshambuliaji hatari wa Ureno, Eusebio, Kevin Keegan aliwabeba tena Waingereza kwa kuwa mshindi wa Ballon d’Or mwaka 1978, kabla ya kuiteta mwaka 1979, wakati huo akiwa mchezaji tishio wa kikosi cha Hamburg ya Ujerumani.

Kama hiyo haitoshi, Waingereza waliibuka tena kidedea kwenye kinyang’anyiro cha Ballon d’Or mwaka 2001 kupitia kwa Michael Owen. Alipata tuzo baada ya kuipa Liberpool mataji matatu [FA, Kombe la Ligi na UEFA Cup].

Related articles

Recent articles