14.7 C
New York

Ronaldo kurudi kikosini Ureno

Published:

LISBON, Ureno

STAA wa soka, Cristiano Ronaldo, anajiandaa kurejea katika kikosi cha timu ya soka ya Taifa ya Ureno.

Kwa wiki za hivi karibuni, mshambuliaji huyo amekuwa kwenye uhusiano mbaya na kocha wake, Jorge Jesus.

Hata hivyo, Jesus amemjumuhisha kwenye kikosi kinachojiandaa kuzikabili Denmark [Novemba 14] na Wales [Novemba 17].

Kutokana na uhusiano wao mbaya, Shirikisho la Soka la Ureno lilimfungia mchezaji huyo kwa siku 30 na kumtoza faini ya euro 255.

Adhabu hiyo ilikuja baada ya ‘CR7’ kuondoka kwa hasira kambini baada ya kugundua hakuwa kwenye mipango ya Jesus kuelekea mechi yao dhidi ya Denmark.

Related articles

Recent articles