23 C
New York

Nini hatima ya mtoto wa Ronaldo?

Published:

LISBON, Ureno

MTOTO wa Cristiano Ronaldo amechagua kuiwakilisha Ureno katika ngazi ya timu ya taifa, licha ya kwamba angeweza kuchagua nchi nyingine.

Cristiano Ronaldo Jr ameichagua Ureno, licha ya kwamba kwa sasa baba yake haelewani na kocha wa timu ya Taifa, Jorge Jesus.

Ugomvi wake na kocha ulianzia pale Ronaldo alipoishia benchi kwa dakika zote 90 za mechi yao ya Ligi ya Mataifa ya Ulaya [UEFA Nations League] dhidi ya Norway siku chache zilizopita.

Hata hivyo, Ronaldo Jr, ambaye ana umri wa miaka 16, ameamua kuiwakilisha Ureno licha ya kwamba angeweza kuchagua mataifa mengine matatu.

Cristiano Jr, wing awa kushoto anayetumia mguu wa kulia, kwa sasa anacheza katika ‘academy’ ya Al-Nassr, klabu anayocheza baba yake huko Saudi Arabia.

Kabla ya hapo, ‘dogo’ huyo aliwahi kupita katika academy za Juventus na Manchester United, ambako pia mzee wake alikuwa anacheza.

Katika ngazi ya timu ya taifa, ameshacheza U-15 na U-16 ya Ureno na kwa mujibu wa takwimu, ameshafunga mabao matano katika mechi 13. Alianza kuitwa Mei, 2026.

Lakini, bado Cristiano Jr ana nafasi ya kuzichagua Hispania alikoishi kwa miaka zaidi ya mitano wakati baba yake akicheza Real Madrid.

Wakati huo huo, kwa kuwa alizaliwa California, Cristiano Jr ana uwezo wa kuchagua kuiwakilisha timu ya Taifa ya Marekani.

Kama hiyo haitoshi, kwa mujibu wa vyanzo vya habari vya Hispania, hasa gazeti la AS, pia kinda huyo ana asili ya Cape Verde lakini hajakidhi vigezo vya FIFA kumuwezesha kuiwakilisha nchi hiyo ya Afrika.

Related articles

Recent articles