14.2 C
New York

Uchaguzi wa rais New Zealand wakosa mshindi

Published:

WELLINGTON, New Zealand

HAKUNA mgombea wa urais aliyefikisha kura za kutosha, hivyo itaundwa serikali ya umoja kati ya chama tawala na upinzani nchini New Zealand.

Katika Uchaguzi uliofanyika jana Novemba 6, 2026, Waziri Mkuu kutoka Chama tawala cha National Party, Christopher Luxon, alipata viti 42 bungeni, akikosa 19 ambavyo vingemfanya kufikisha idadi inayohitajika ili kuunda serikali.

Hivyo, Luxon wa National Party atashirikiana na wagombea wenzake wa vyama vya Labour, ACT na New Zealand First kuunda serikali ya mseto.

Kampeni za Uchaguzi wa mwaka huu wa New Zealand ziligubikwa na hoja nzito za kupanda kwa gaharama za maisha na uhaba wa ajira kwa vijana walio wengi.

Aidha, kwa wachambuzi wa siasa, matokeo hayo ya kukosekana kwa mshindi ni ishara ya wananchi kutaka mabadiliko makubwa na ya haraka katika siasa za New Zealand.

Related articles

Recent articles