LAGOS, Nigeria
LEJENDARI wa timu ya soka ya Taifa ya Nigeria ‘Super Eagles’, Austin ‘Jay-Jay’ Okocha, amezitaja Barcelona, Manchester City na Bayern Munich kuwa ndizo zenye uwezo wa kutwaa ubingwa msimu huu wa Ligi ya Mabingwa Ulaya.
Wakati huo huo, Okocha aliyewahi kuwika Ligi Kuu ya England akiwa na Bolton, amemtabiria staa wa Real Madrid, Kylian Mbappe, tuzo ya mwaka huu ya Ballon d’Or.
Okocha alifanya utabiri wake huo katika mahojiano yake na jarida la Le Journal du Dimanche la Ufaransa.
Utabiri wake kwa Mbappe umekuja wakati mshambuliaji huyo akikabiliwa na upinzani mkali kutoka kwa Harry Kane, Mbappe na Lamine Yamal.
Hata hivyo, Okocha anaamini Mbappe ana nafasi kubwa zaidi kutokana na kiwango chake bora katika michuano ya Kombe la Dunia, Ligi ya Mabingwa Ulaya na La Liga msimu uliopita.
“Nafikiri Mbappe anastahili kwa kuwa alikuwa mfungaji bora wa Kombe la Dunia (10), Ligi ya Mabingwa (15) na La Liga (25),” amesema.


