15.1 C
New York

Nani kuvaa viatu vya Harry Kane?

Published:

LONDON, Uingereza

KWA miaka ya hivi karibuni, Harry Kane si tu amekuwa nahodha, bali pia mchezaji muhimu zaidi kwenye safu ya ushambuliaji ya timu ya soka ya Taifa ya England ‘Three Lions’.

Hata hivyo, akiwa tayari ana umri wa miaka 33, ni wazi sasa mashabiki wa England wameshaanza kujiuliza ni nani atarithi mikoba yake endapo mfungaji bora huyo wa muda wote wa timu hiyo atastaafu?

Will Lankshear

Kinda mweye umri wa miaka 21 na sasa anakipiga Middlesbrough akitokea Tottenham iliyomuuza kwa mkataba wenye kipengele kinachowaruhusu kumrejesha hapo baadaye.

Tangu alipojiunga na M’sbrough majira ya kiangazi, 2026, Lankshear ameshafunga mabao nane katika mechi 11. Alifunga bao katika mechi ya kwanza tu akiwa na ‘uzi’ wa U-21 ya England.

Msimu huu wa Ligi Daraja la Kwanza nchini England [Championship], ameshapachika mabao sita katika dakika 678 alizocheza.

Brian Madjo

Amechagua kuiwakilisha England badala ya Luxembourg alikokulia. Agosti, 2026, Madjo [17], alifunga bao katika mechi yake ya kwanza akiwa na Aston Villa [dhidi ya PSG].

Licha ya kuandamwa na majeraha, kinda huyo ameshacheza mechi tisa akiwa na jezi za U-17 ya England. Kiwango chake kitampa muda mwingi wa kucheza pale Aston Villa.

Shim Mheuka

Kinda wa Chelsea ambaye ameshafunga mabao 26 katika mechi 39 za timu za vijana. Umri wake ni miaka 18 na kwa sasa anacheza kwa mkopo Celtic akitokea Stamford Bridge.

Wakati huo huo, Mheuka ameshapachika mabao 16 katika michezo 23 ya U-19 ya England. Ndiye aliyefunga bao wakati U-20 ya England ilipoifunga Ufaransa hivi karibuni.

Alejandro Gomes Rodriguez

Alizaliwa Venezuela na ana asili ya Ureno lakini amechagua kuiwakilisha England. Ni mshambuliaji wa Lyon ya Ligi Kuu ya Ufaransa [Ligue 1] na umri wake ni miaka 18 tu.

Nyota huyo wa zamani wa Southampton alianza kuitumikia U-19 ya England wiki chache zilizopita. Pia, ameshacheza mechi 23 za U-17 na U-18.

Msimu uliopita, alipata nafasi ya kucheza mechi tano za Lyon katika michuano ya Ligi ya Europa. Ana mabao mawili katika mechi 13 za Ligi Daraja la Pili ya Ufaransa [Ligue 2].

Related articles

Recent articles