LONDON, Uingereza
BEKI Nicolas Otamendi amekuwa staa mwingine kutangaza kustaafu kuitumikia timu ya soka ya Argentina baada ya Lionel Messi.
Otamendi alikuwa kikosini wakati Messi anacheza mechi yake ya mwisho hivi karibuni, ambapo Argentina ilishinda mabao 3-0 dhidi ya Benin.
Otamendi mwenye umri wa miaka 38, alikuwa sehemu ya kikosi wakati Argentina inatwaa Copa America mwaka 2021 na 2024.
Pia, beki huyo wa zamani wa Manchester City alicheza mechi zote wakati timu hiyo inatwaa ubingwa wa Kombe la Dunia mwaka 2022.
Katika mechi ya kumuaga Messi, Otamendi anayekipiga River Plate ya Argentina ndiye aliyefunga bao la kwanza, kisha akatoa pasi kwa Messi aliyetoa asisti kwa bao la pili la Nico Paz.


