CAIRO, Misri
NI nchi 20 pekee kutoka barani Afrika zitakazopewa nafasi ya kupiga kura katika kinyang’anyiro cha tuzo ya Mchezaji Bora ya Ballon d’Or.
Nafasi hiyo imepatikana kwa kuwa nchi hizo za Afrika zimo ndani ya ‘Top 100’ ya viwango vya ubora wa soka vya Shirikisho la Soka la Kimataifa [FIFA].
Kwa mujibu wa waandaaji wa tuzo, nchi za Afrika zilizopata nafasi hiyo ni Morocco inayoshika nafasi ya sita duniani, Senegal [18], Misri [24], Nigeria [26], na Algeria [29].
Nchi zingine ni Ivory Coast [31], DRC [41], Cameroon [43], Mali [53], Afrika Kusini [54], Tunisia [57], Burkina Faso [62], Cape Verde [64], Ghana [65], Guinea [81na Gabon [84], Angola [87], Uganda [89], Zambia [90], na Benin [94].
Wakati huo huo, nchi zingine 80 zitakazopiga kura zinatoka katika mabara ya Ulaya, Asia, Amerika ya Kaskazini na Kusini na Oceania.


