MADRID, Hispania
KOCHA wa Real Madrid, Jose Mourinho, yuko tayari kumtema kwenye kikosi cha kwanza mshambuliaji wake raia wa Brazil, Vinicius Junior.
Kwa mujibu wa Gazeti la Marca la Hispania, Mourinho aliyeajiriwa wiki chache zilizopita amechoshwa na winga huyo.
Vinicius alihusishwa kujiunga na Arsenal wakati wa usajili wa dirisha kubwa la kiangazi, mwaka huu, lakini dili hilo lililota mbawa na kubaki Madrid.
Hata hivyo, nyota huyo mwenye umri wa miaka 26 hajauanza vizuri msimu huu wa 2026-27 kwani amefunga bao moja pekee katika mechi zake nane.
Katika mchezo uliopita wa La Liga dhidi ya Atletico Madrid, Mourinho alimwita benchi katika dakika ya 54 na Madrid kufungwa mabao 2-1.


