20.1 C
New York

Lipia kwa awamu ili uunganishiwe umeme

Published:

Na Hassan Mwasha, Gazetini

WAKATI mwingine, kama inavyoanishwa katika Mkataba wa Huduma kwa Wataje, TANESCO inatoa nafasi wa wananchi wenye uchumi mdogo kumudu gharama za nishati hiyo.

Moja ya njia ilizonazo katika kumuwezesha ‘mwananchi wa kawaida’ kutotengwa na matumizi ya umeme ni namna ilivyomuweka mfumo wa malipo ya awamu tatu mteja aliyepokea makadirio ya gharama za kulipia.

Kama ilivyoelezwa vizuri katika Mkataba huo wa Huduma kwa Wateja, baada ya kupokea makadirio ya gharama, mteja anayetaka kuunganishiwa umeme kwa malipo ya awamu ataomba na kuingia mkataba na TANESCO.

TANESCO, kwa upande wake, itamruhusu awamu za malipo zisizozidi tatu kwa miezi mitatu mfululizo. Mathalan, kama makadirio gharama ni laki tatu na ishirini na moja, basi aweze kulipa mara tatu tu ndani ya kipindi hicho cha miezi mitatu.

Hata hivyo, imeanishwa katika Mkataba kuwa ile awamu ya kwanza itapaswa kujumuhisha malipo yote ya Kodi ya Ongezeko la Thamani [VAT].

Pia, mteja atakayeshindwa kulipia kiasi chote cha gharama ndani ya miezi mitatu hiyo atawajibika kulipia gharama za ziada endapo kutatokea ongezeko la gharama katika kipindi hicho.

Wakati huo huo, mteja atafahamishwa kuwa zoezi la kuunganishiwa umeme halitofanyika hadi pale atakapokuwa amemaliza kulipa kiasi chote. Na si kwamba atawekewa umeme wakati akiendelea kulipa.

Kwa maelezo zaidi, unaweza kuwasiliana na Kituo cha Huduma kwa Wateja cha TANESCO kupitia nambari 180 [bure].

Related articles

Recent articles