26.3 C
New York

Relie M atamba na ‘Gospel Hip hop’ East Africa

Published:

Douala, Cameroon

MMREMBO anayekuja kwa kasi kwenye muziki wa Injili nchini Cameroon, Relie M, amewakosha wapenzi wa muziki huo baada ya kuachia wimbo mpya wenye ladha ya Hip Hop.

Katika wimbo huo unaoitwa Only Jesus Know, Relie M ameonyesha kipawa chake kingine cha kurap huku akieneza Injili kwa mtindo huo na ndani ya muda mfupi umepokewa vizuri na mashabiki Afrika Mashariki.

“Only Jesus Know imenifungulia njia zaidi huko Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Nimepata idadi kubwa ya watazamaji kwenye chaneli yangu ya YouTube, naamini mashabiki wanaendelea kunipa sapoti ili kwa pamoja muziki wetu ufike mbali,” amesema Relie M.

Binti huyo mdogo anayekuja kwa kasi kwenye muziki wa Injili barani Afrika anasimamiwa na Rim Plug ya Rene Immortal chini ya lebo ya Queen Light Music.

Related articles

Recent articles