LONDON, Uingereza
MSHAMBULIAJI wa zamani wa Arsenal, Theo Walcott, ameitaja Liverpool kama timu anayoona itawapa ushindani mkali katika mbio za ubingwa wa Ligi Kuu ya England msimu huu wa 2025-26.
Akitoa maoni yake katika mahojiano na kituo cha televisheni cha BBC Sport, Walcott amesema anaamini hivyo kutokana na ubora wa kocha mpya wa Liverpool, Andoni Iraola.
Kwa mtazamo wake, Iraola atawarejesha kwa kiwango bora mastaa wawili walioshindwa kung’ara Anfield, Alexander Isak na Florian Wirtz.
“Liverpool ni moja ya timu ngumu. Iraola ni kocha mzuri, na huenda Alexander Isak na Florian Wirtz wakawa na msimu mzuri,” amesema.
Arsenal walimaliza msimu uliopita (2025-26) wakiwa mabingwa wa EPL, ambapo Liverpool walishuka nafasi ya tano kwenye msimamo.


