CATALUNYA, Hispania
IMEFICHUKA kuwa uongozi wa klabu ya Barcelona unaangalia uwezekano wa kumrejesha kundini mshambuliaji wake tishio, Robert Lewandowski.
Lewandowksi aliyeondoka Barcelona majira haya ya kiangazi, kwa sasa amejiunga na klabu ya Chicago Fire.
Kwa mujibu wa mwandishi wa habari wa Italia, Fabrizio Romano, Barcelona imeanza kuwasiliana na klabu hiyo ya MLS (Ligi Kuu ya Marekani).
Kupitia ukurasa wake wa X, Romano alisema: “Barcelona wameanza mazungumzo rasmi na ya kumrudisha Robert Lewandowski.”
“Hansi Flick (kocha wa Barcelona) yuko tayari kwa asilimia 100 kwa Lewandowski kurudi, kwa mkataba wa msimu mmoja. Hakuna ofa iliyopelekwa, lakini ni ‘Plan B’ ya Barcelona.”


