Na mwandishi wetu, Gazetini
SEKTA ya Uchumi wa Buluu unaozingatia matumizi endelevu ya rasilimali za bahari na maji baridi, utakuwa na mchango mkubwa katika kuleta maendeleo nchini.
Tanzania ambayo ina Ukanda mrefu wa pwani, maziwa na mito mikubwa ina fursa nyingi za kukuza sekta ya uvuvi, utalii wa pwani na wa maziwa, usafiri wa mjini, na matumizi ya nishati mbadala kutoka baharini.
Ukweli unaothibitishwa na tafiti unaonesha kuwa sekta hizi zina nafasi kubwa ya kuongeza ajira, kukuza mapato, na kuhifadhi mazingira.
Ili nchi iweze kutumia fursa hizi kikamilifu, itakuwa muhimu kuwekeza katika gesi asilia, uhifadhi wa bahari, uvuvi endelevu, na ujenzi wa miundombinu.
Hatua za kimkakati katika gesi asilia, uendelezaji wa bahari na upanuzi wa nishati ya kutumia wa maji zinachangia mpango madhubuti wa kutumia kikamilifu fursa za uchumi wa buluu hapa nchini.


