NEW YORK, Marekani
TIMU ya soka ya Taifa ya Ujerumani imeungana na zingine mbili kutinga hatua ya 32 Bora ya fainali za Kombe la Dunia za mwaka huu.
Ujerumani wamevuka wakiwa Kundi E baada ya ushindi wao wa mabao 2-1 walioupata mbele ya Ivory Coast.
Itakumbukwa kuwa vijana hao wa kocha mzawa, Julian Nagelsmann, walishashinda mechi ya kwanza dhidi ya ‘vibonde’ Curacao.
Ivory Coast walitangulia kwa bao la kiungo wa zamani wa Barcelona, Franck Kessie, kabla ya Deniz Undav kufunga mawili alitokea benchi.
Ni kwa maana hiyo, Ujerumani sasa inaungana na wenyeji wawili, Mexico na Marekani, ambao nao wametinga hatua inayofuata (32 Bora).


