HAVANA, Cuba
SERIKALI ya Marekani imetangaza vikwazo vya kiuchumi dhidi ya Rais wa Cuba, Miguel Diaz-Canel, pamoja na familia yake.
Taarifa ya vikwazo hivyo pia inaihusu familia ya Rais wa zamani wa Cuba, Raul Castro, licha ya kwamba kwa sasa hayuko madarakani.
Hatua hiyo ni mwendelezo wa Marekani kuitunishia misuli Cuba katika ugomvi wao wa miaka mingi. Marekani imetishia mara kadhaa kukivamia Kisiwa hicho jirani.
Rais Diaz-Canel, mkewe na mtoto wake wa kiume wamewekewa vikwazo, adhabu hiyo ikiigusa pia jeshi la Cuba na taasisi zingine.
Cuba imekuwa ikipambana na vikwazo vya kiuchumi vya Marekani tangu mwaka 1962, lakini miezi ya hivi karibuni imemshuhudia Rais Donald Trump akiiongezea presha zaidi.
Mbali ya kutangaza nia ya kuivamia kijeshi, amezuia kuingia kwa mafuta Cuba, huku akizitangazia vita nchi zinazofanya biashara na Kisiwa hicho.


