25.2 C
New York

Di Maria: Ronaldo, Messi hawatishi tena

Published:

MADRID, Hispania

WINGA wa zamani wa Real Madrid, Angel Di Maria, amesema zama za Cristiano Ronaldo na Lionel Messi kutawala mijadala ya soka zimekwisha.

Di Maria amekuja na maoni hayo alipokuwa akizungumzia uwezekano wa mastaa hao kutwaa tuzo ya Ballon d’Or baada ya kumalizika kwa fainali za Kombe la Dunia za mwaka huu.

Ronaldo wa Ureno na Messi kwa upande wa Argentina, kila mmoja atashiriki Kombe la Dunia kwa mara ya sita msimu huu michuano hiyo itakapofanyika Marekani, Canada na Mexico.

Kama ilivyo kawaida, mataifa hayo yanapewa nafasi kubwa ya kutwaa ubingwa wa fainali hizo zitakazoanza Juni 11, 2026.

Katika mahojiano yake na tovuti rasmi ya Ballon d’Or, Di Maria raia wa Argentina amesema: “Ni kawaida (wawili hao kuhusishwa na Ballon d’Or) lakini kwa sasa zama zao kimekwisha.”

Related articles

Recent articles