30.7 C
New York

Slot atupa dongo Liverpool, asema ameiacha inapostahili

Published:

MERSEYSIDE, Uingereza

KOCHA wa Liverpool, Arne Slot, amefunguka kwa mara ya kwanza tangu alipofukuzwa klabuni hapo Jumamosi ya wiki iliyopita (Mei 30, 2026).

Slot, raia wa Uholanzi mwenye umri wa miaka 47, amesema ameondoka na kuiacha Liverpool pale inapostahili, yaani moja ya klabu kubwa za soka barani Ulaya.

Kauli hiyo inaweza isiwafurahishe mashabiki na hata mabosi wa Liverpool kwani walimtimua wakati wamemaliza msimu wakiwa nafasi ya tano kwenye msimamo wa Ligi Kuu ya England.

Wakati huo huo, Liverpool ilimaliza msimu huo wa 2025-26 ikiwa imeachwa pointi 25 na timu iliyotwaa ubingwa, Arsenal.

Hata hivyo, Slot haoni ubaya wowote kwani Liverpool itashiriki Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu ujao.

“Kufuzu Ligi ya Mabingwa lilikuwa jukumu la msingi, ambalo linaipa Liverpool uhakika wa kushindana katika soka la daraja la juu msimu ujao,” amesema.

Related articles

Recent articles