RABAT, Morocco
LICHA ya kufungwa na Senegal, bado timu ya soka ya vijana wa U-17 ya Tanzania ‘Serengeti Boys’ ina tiketi ya kushiriki fainali za Kombe la Dunia za mwaka huu.
Katika mchezo huo wa fainali ya AFCON uliochezwa jana Juni 2, 2026, Serengeti Boys ilipoteza kwa kichapo cha penalti 4-2 baada ya dakika za uwanjani kumalizika kwa sare ya bao 1-1.
Mbali ya tiketi ya Kombe la Dunia, michuano itakayochezwa mwishoni mwa mwaka huu nchini Qatar, Serengeti Boys imeweka rekodi ya kuingia kwa mara ya kwanza hatua ya fainali ya AFCON.
Katika hatua ya robo na nusu fainali, Serengeti Boys ilionesha ubora mkubwa kwa kuzitoa timu ngumu za Algeria na Misri.
Senegal, kwa upande wao, ambao waliingia fainali kwa kuwatoa wenyeji Morocco, wametwaa kwa mara ya pili ubingwa wa AFCON ya vijana wa umri chini ya miaka 17.


