19.8 C
New York

Mgombea urais wa zamani Venezuela ataka Uchaguzi Mkuu

Published:

CARACAS, Venezuela

ALIYEWAHI kuwa mgombea wa urais wa upinzani nchini Venezuela, Edmundo Gonzalez Urrutia, ametaka kufanyika kwa Uchaguzi Mkuu ikiwa ni miezi mitano imepita tangu Rais Nicolas Maduro alipoondoshwa madarakani na jeshi la Marekani.

Gonzalez ni mwanasiasa maarufu wa Venezuela, akiwahi pia kuwa balozi wa nchi hiyo katika nchi za Algeria na Argentina.

Urrutia (76), aliwania kiti cha urais dhidi ya Maduro katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2024, ambapo hata hivyo alishindwa.

Hata hivyo, licha ya Maduro kushinda kwa idadi ya kura, mataifa mengi yalimpinga na kumtambua Urrutia kama mshindi wa Uchaguzi huo.

Kwa sasa, Venezuela iko chini ya Serikali ya Mpito akiiongozwa na mshindi wa tuzo ya Amani ya Nobel, Maria Corina Machado

Kwa upande wake, Urrutia hamuungi mkono Machado, licha ya kwamba ni mwenzake katika siasa za upinzani nchini humo.

Related articles

Recent articles