27 C
New York

Yanga yaibamiza Namungo, yarudi kileleni ikiisubiri Mashujaa

Published:

Na Hassan Mwasha, Gazetini

YANGA imerejea kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu Bara bada ya ushindi mnono wa mabao 3-1 walioupata mbele ya Namungo katika mchezo wa leo Mei 25, 2026.

Katika mchezo huo uliochezwa kwenye Uwanja wa KMC, Mwenge jijini Dar es Salaam, Yanga ilipata mabao yake kupitia kwa Duke Abuya (dk. 26) na Allan Okelo aliyefunga mawili (dk. 53 na dk. 85).

Kwa matokeo hayo, Wanajangwani wamerudi kileleni baada ya kuifikisha pointi 60, wakiizidi mbili Simba inayoshika nafasi ya pili, huku kila timu ikiwa imecheza mechi 25.

Katika mwendelezo wa Ligi, Yanga watashuka tena dimbani Juni 13, 2026 kumenyana na Mashujaa mkoani Kigoma, kisha Simba watacheza siku inayofuata dhidi ya Pamba, mchezo utakaochezwa kwenye Uwanja wa KMC.

Related articles

Recent articles