27 C
New York

Simanzi! Spurs kuaga EPL baada ya miaka 34?

Published:

LONDON, Uingereza

TOTTENHAM ni moja ya zile klabu sita zilioasisi Ligi Kuu ya England (EPL) na imeshiriki kwa miaka yote 34 ya michuano hiyo ya soka.

Timu zingine tano ambazo hazijawahi kuonja machungu ya kushuka daraja ni Arsenal, Manchester United, Liverpool, Chelsea na Everton.

Hata hivyo, msimu huu mambo ni magumu kwa Tottenham na huenda ikaiaga Jumapili ya wikiendi hii pazia la Ligi litakapofungwa.

Kuelekea mechi yake ya mwisho dhidi ya Everton, ambapo Tottenham itakuwa nyumbani, vijana hao wa kocha Roberto De Zerbi wanashika nafasi ya 17 katika msimamo wa EPL.

Ni mechi ambayo Tottenham inatakiwa kushinda ili kubaki Ligi. Kinyume chake, kama watafungwa, kisha West Ham ikaifunga Leeds, basi majirani zao hao wa London ndiyo watakaobaki Ligi Kuu.

Aston Villa, ambayo pia ni moja ya klabu zilizoasisi EPL, ilishuka daraja msimu wa 2015-16, kabla ya kurejea na sasa iko ndani ya ‘Top 4’ na imetoka kunyakua ubingwa wa Ligi ya Europa hivi karibuni.

Related articles

Recent articles