LONDON, Uingereza
ASTON Villa ndiyo Mabingwa wa msimu huu wa 2025-26 wa michuano ya Ligi ya Europa. Hata hivyo, kwa kuifunga Freiburg mabao 3-0 katika mchezo wa fainali, ni ubingwa wao wa kwanza wa mashindano hayo.
Historia inaitambua Sevilla ya La Liga kuwa ndiyo timu inayoongoza kwa kutwaa mara nyingi (7) taji la mashindano hayo ya Shirikisho la Soka barani Ulaya (UEFA).
Katika nafasi ya pili, ni klabu za Inter Milan, Liverpool, Juventus, Atletico Madrid na Tottenham, ambazo kila moja imebeba mara tatu.
Nafasi ya tatu inashikwa na Borussia Monchengladbach, Feyenoord, IFK Göteborg, Real Madrid, Parma, Porto, Chelsea na Eintracht Frankfurt, kila moja ikiwa na ‘ndoo’ mbili za Ligi ya Europa.
Timu zinazofuata, ambazo ni Villa, Anderlecht, Ajax, Man United, PSV Eindhoven, Ipswich Town, Leverkusen, Napoli, Bayern Munich, Schalke, Galatasaray, Valencia, CSKA Moskva, Zenit, Shakhtar, Villarreal na Atalanta zimetwaa ubingwa mara moja kila moja.


