WASHINGTON DC, Marekani
SAKATA la mtuhumiwa wa tukio la kufyatua risasi katika halfa aliyokuwemo Rais Donald Trump limechukua sura mpya.
Mwanaume huyo mwenye umri wa miaka 31, Cole Tomas Allen, alifanya tukio hilo jirani na walinzi wa Rais Trump katika hafla iliyoandaliwa na waandishi wa Habari za Ikulu mjini Washington.
Kwa mujibu wa Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Tomas Allen alilenga kuwadhuru viongozi wa Marekani waliokuwamo ukumbini.
Katika barua aliyoiachia familia kabla ya kwenda kwenye tukio, Allen alisema yeye ni adui wa sera za kiongozi huyo.
Ujumbe wake kwa familia uligusia pia alivyokwerwa na hatua ya Rais Trump kuzishambulia boti alizodai kuwa ni za dawa za kulevya katika Bahari ya Pacific.


