9.5 C
New York

Simbu ang’ara tena Boston Marathon, ashika nafasi ya pili

Published:

Na Mwandishi Wetu

Mwanariadha nyota wa Tanzania, Sajinitaji Alphonce Simbu, ameendelea kufanya vizuri Boston Marathon baada ya kushika nafasi ya pili kwa mwaka wa pili mfululizo.

Katika mbio hizo zilizofanyika leo Jumatatu, Aprili 20, 2026, Boston, Marekani, Simbu amekimbia kwa muda wa 2:02:47, muda huo unamfanya mwanariadha huyo kuweka rekodi mpya ya Taifa.akivunja rekodi yake ya awali ya 2:04:38 aliyoiweka mwaka 2024.

Nafasi ya kwanza imechukuliwa na Mkenya John Korir aliyetumia muda wa 2:01:52, akitetea ubingwa wake, namba tatu ni Benson Kipruto wa Kenya alikimbia kwa muda wa 2:02:50.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img