18.1 C
New York

Eritrea wana historia yao AFCON 2027

Published:

CAIRO, Misri

BAADA ya miaka 19 kupita, timu ya soka ya taifa ya Eritrea imerejea katika hatua ya makundi ya kufuzu fainali zijazo za AFCON zitakazofanyika hapo mwakani.

Eritrea imeingia makundi ya kufuzu baada ya kuifunga Eswatini jumla ya mabao 4-1 katika mechi mbili (nyumbani na ugenini) za hatua ya awali.

Mshambuliaji anayekipiga Kahrabaa Ismaila ya Misri, Ali Sulieman, ndiye shujaa wao kwani alifunga mabao matatu kati ya manne.

Kwa kukosa uwanja unaokidhi vigezo vya FIFA, Eritrea walitumia Morocco kwa mechi zao za nyumbani.

Katika mechi ya kwanza, ambapo walishinda mabao 2-0 dhidi ya Eswatini, walipata mabao yao kupitia kwa Sulieman na Siem Eyob-Abraha anayekipiga Sheffield United ya England.

Safari hii, walijihakikishia tiketi ya kwenda makundi ya kufuzu baada ya kuifunga Eswatini mabao 2-1.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img