6.4 C
New York

Senegal walifikisha jambo lao CAS

Published:

NYON, Uswis

MAHAKAMA ya Kimataifa ya Usuluhishi wa Michezo (CAS) imekiri kupokea malalamiko ya Shirikisho la Soka la Senegal.

FSF wamefikisha ombi la kupinga kile kilichofanywa na Shirikisho la Soka Afrika (CAF) wiki chache zilizopita.

Katika mazingira yaliyoacha maswali, CAF waliivua Senegal ubingwa wa fainali za AFCON 2025 na kuukabidhi kwa Morocco.

Adhabu hiyo ilitokana na kitendo cha wachezaji wa Senegal kutishia kugomea mchezo wa fainali uliochezwa Januari 18, 2026.

Hatua yao ya kugomea kwa dakika zaidi ya 10, ikiwamo kuingia vyumbani, ilitokana na kutokubaliana na penalti waliyopewa Morocco, ambayo hata hivyo haikuwapa bao wenyeji hao.

Licha ya hatimaye Senegal kushinda bao 1-0 na kutwaa ubingwa, siku chache zilizopita CAF ‘walipindua meza’ na kuipokonya ubingwa.

“Rufaa ya FSF ni kupinga uamuzi wa CAF ili warejeshewe ubingwa wa AFCON. Jopo la CAS litakaa ili kubadili suala hili,” imeeleza taarifa ya CAS.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img