9.5 C
New York

Mshahara haukupi utajiri, mwajiriwa zinduka mapema

Published:

Na Benjamin Madaha

WAFANYABIASHARA, vijana na hata waajiriwa kuna kanuni moja ya uchumi wa kipato ambayo watu wengi hawaielewi mapema.

Utajiri haujengwi kwa kipato cha mara moja kwa mwezi. Unajengwa kwa mifumo ya pesa inayoingia kila siku.

Watu wengi wana mfumo huu. Wanatumia pesa kila siku lakini wanaingiza pesa mara moja kwa mwezi.

Hapo ndipo tatizo linaanzia. Kwa sababu mshahara ni mfumo unaoitwa ‘fixed income’.

Unajua kabisa tarehe ya kulipwa, kiasi cha kulipwa na mwisho wake. Mfumo huu unakuwa ‘limited’ na ‘calculated’.

Ukilipwa mara 12 kwa mwaka, hata ukifanya kazi kwa bidii kiasi gani, mfumo wa kipato chako bado umewekewa ukomo.

Ndiyo maana watu wengi wanafanya kazi miaka 20–30 lakini bado hawajafikia uhuru wa kifedha.

Matajiri wengi hutumia mfumo tofauti. Wanajenga kile kinachoitwa ‘daily cash flow system’ (mfumo wa kuingiza kipato kila siku).

Yaani pesa inaweza kuingia kila siku, kila wiki na kutoka vyanzo tofauti. Mfano wa mifumo ya pesa ya kila siku ni ipi?

Biashara: Biashara inaweza kuuza kila siku. Hata kama ni faida ndogo, lakini inaingia mara nyingi.

Huduma (services): ‘Consulting’, ‘design’, ‘marketing’, ‘IT’, ‘training’ – hizi zinaweza kuleta wateja mara kwa mara.

Digital income (kipato mitandaoni): Internet imeleta mfumo wa kipato cha kila siku kupitia online services, digital products, affiliate marketing na freelancing.

‘Assets’ zinazozalisha pesa: Mfano nyumba za kupangisha, mashine za uzalishaji na mitandao ya biashara.

Hizi zinaweza kuleta kipato bila kusubiri mwisho wa mwezi. Kuna kanuni muhimu sana hapa.

‘Wealth is built by frequency of income, not just size of income’. Yaani utajiri haujengwi tu na pesa nyingi, unajengwa na mara ngapi pesa inaingia.

Hata kama una ajira, fikiria kimkakati. Ni mfumo gani unaweza kukuletea pesa kila siku au kila wiki?

Kwa sababu ukweli ni huu; mshahara unaweza kukusaidia kuishi, lakini mifumo ya ‘cash flow’ ndiyo inajenga utajiri

Mwalimu Benjamin Madaha ni mchambuzi mbobezi wa masuala ya fedha.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img