18.5 C
New York

Morocco yatwaa ubingwa wa AFCON 2025 baada ya CAF kubatilisha matokeo ya fainali

Published:

Na mwandishi wetu, Gazetini

TIMU ya taifa ya Morocco imetangazwa kuwa mabingwa wa Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON 2025) kufuatia uamuzi wa Shirikisho la Soka Afrika (CAF) kubatilisha matokeo ya awali ya fainali dhidi ya Senegal na kuipa ushindi wa mezani.

Awali, Senegal iliibuka na ushindi wa bao 1-0 katika fainali iliyochezwa Januari 18 jijini Rabat, Morocco. Hata hivyo, mchezo huo ulikumbwa na sintofahamu baada ya wachezaji wa Senegal kususia kuendelea kucheza wakipinga maamuzi ya mwamuzi, ikiwemo penati iliyotolewa dakika za mwisho wakati matokeo yakiwa 0-0.

Baada ya kusimama kwa takribani dakika 17, wachezaji wa Senegal walirejea uwanjani kufuatia kushawishiwa, ambapo penati ya Morocco iliyopigwa na Brahim Diaz iliokolewa na kipa Edouard Mendy kabla ya Senegal kufunga bao la ushindi kupitia Pape Gueye katika muda wa nyongeza.

Hata hivyo, Morocco iliwasilisha rufaa CAF ikipinga mwenendo wa mchezo huo. Katika uamuzi uliotolewa siku 58 baadaye, CAF imesema Senegal ilikiuka kanuni za mashindano na hivyo “inachukuliwa kupoteza mchezo huo kwa kufungwa mabao 3-0.”

Kutokana na uamuzi huo, Morocco imetangazwa bingwa wa AFCON 2025, huku CAF pia ikitoa adhabu mbalimbali ikiwemo faini kwa pande zote mbili. Uamuzi huo umeibua mjadala mkubwa na kuingia katika historia ya soka la Afrika kama moja ya maamuzi yenye utata mkubwa.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img