15.6 C
New York

Mabosi wa Liverpool kumpa mikoba Alonso

Published:

MERSEYSIDE, Uingereza

KUNA uwezekano mkubwa huu ukawa msimu wa mwisho kwa kocha raia wa Uholanzi, Arne Slot, kuliongoza benchi la ufundi la Liverpool.

Wamiliki wa klabu hiyo, FSG, wanajadili hatima yake, huku jina la Xabi Alonso likitajwa kuwa mezani kwao.

Slot alikuwa na wakati mzuri katika msimu wake wa kwanza Anfield, ambapo aliipa taji la Ligi Kuu, lakini safari hii mambo ni magumu kwa upande wake.

Licha ya kutumia Pauni milioni 440 katika soko la usajili wa kiangazi, 2025, Liverpool imeonekana kushuka kiwango, ikiandamwa na tatizo la kukosa mwendelezo wa matokeo mazuri.

Mabosi wa Anfield wameripotiwa kukerwa zaidi na kichapo cha mabao 2-1 walichokipata katika mchezo uliopita dhidi ya Wolves.

Ni kutokana na mwenendo huo, Liverpool wanaamini Alonso, ambaye ni kiungo wao wa zamani, anaweza kuwa mtu sahihi wa kuchukua nafasi ya Slot.

Alonso raia wa Ujerumani, amekuwa nje ya kazi ya ukocha kwa miezi takribani mitatu tangu alipofungashiwa virago na vigogo wa La Liga, Real Madrid.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img