LONDON, Uingereza
KLABU ya Arsenal imeanza harakati za kumsajili moja kwa moja beki wake wa mkopo, Piero Hincapie.
Nyota huyo mwenye umri wa miaka 24, amekuwa na kiwango bora tangu alipotua Emirates akitokea Bayern Leverkusen mwaka jana.
Baada ya kiwango kizuri katika mchezo uliopita dhidi ya Brighton, mashabiki wa Arsenal walitumia mitandao ya kijamii kuwaomba viongozi wambakize klabuni hapo.
Uongozi wa Arsenal umepanga kutenga Pauni milioni 45 ili kuishawishi Leverkusen ya Bundesliga ikubali kumwachia.
Njia hiyo ndiyo waliyoitumia Washika Bunduki kwa David Raya, ambapo walimchukua kwa mkopo kutoka Brighton, kabla ya kumsajili moja kwa moja.


