20.9 C
New York

Kocha afukuzwa kazi timu yake ikishinda 8-0

Published:

RIO, Brazil

KLABU ya Flamengo ya Brazil imetangaza kumfuta kazi kocha wake, Filipe Luis. Ni baada ya timu hiyo kushinda mabao 8-0 dhidi ya Madureira.

Flamengo ilitangaza uamuzi wake saa chache tu baada ya ushindi huo wa nusu fainali ya Kombe la Ligi (Campeonato Carioca).

Kabla ya mchezo huo, itakumbukwa kuwa Flamengo ilitoka kupoteza mechi mbili mfululizo dhidi ya Corinthians na Lanus.

Luis aliyewahi kucheza soka barani Ulaya akiwa na Chelsea na Atletico Madrid, anaondoka Flamengo baada ya kuiongoza katika mechi 101, akishinda 64 na kufungwa 15.

Kwa miaka miwili, 2024 na 2025, aliifanya Flamengo kuwa timu tishio, ambapo ilitwaa mataji makubwa matatu; Copa do Brasil, Brasileirao na CONMEBOL Libertadores.

Related articles

Recent articles