9.8 C
New York

Diaz aandika historia mpya AFCON

Published:

RABAT, Morocco

MSHAMBULIAJI wa timu ya taifa ya Morocco, Brahim Díaz, amekuwa mchezaji wa kwanza katika historia ya fainali za Mataifa Afrika (AFCON) kufunga bao katika mechi tano mfululizo.

Diaz (26), ameandika historia hiyo baada ya kupachika bao moja wakati Morocco ilipoitandika Cameroon mabao 2-0 usiku wa jana Januari 9, 2026.

Timu kongwe hizo katika soka la Afrika zilicheza mchezo wa robo fainali ya michuano ya msimu huu ya AFCON (AFCON 2025).

Ikumbukwe, nyota huyo alifunga bao moja katika mechi zote tatu za hatua ya makundi dhidi ya Comoro, Mali na Zambia.

Katika mchezo wa hatua ya 16 Bora, Diaz aliingia tena kambani, safari hii akizifumania nyavu za Tanzania. Alifunga dakika ya 86.

Tangu alipoipa kisogo Hispania na kuamua kuiwakilisha Morocco, mshambuliaji huyo ameifungia mabao 13 katika mechi 20.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img