11.8 C
New York

Osimhen, Salah watinga robo fainali AFCON 2025

Published:

RABAT, Morocco

MABAO mawili ya Victor Osimhen yameiwezesha timu ya taifa ya Nigeria ‘Super Eagles’ kupata ushindi wa 4-0 dhidi ya Msumbiji katika mchezo wa hatua ya 16 Bora ya fainali za AFCON 2025.

Katika mtanange huo wa kusaka tiketi ya robo fainali uliochezwa jana Januari 5, 2025, mabao mengine ya Super Eagles yalifungwa na Ademola Lookman, ambaye pia alitoa ‘asisti’, na Akor Adams.

Wakati huo huo, staa wa Liverpool, Mohamed Salah, naye aliiongoza timu yake ya taifa ya Misri kufuzu hatua ya robo fainali ya michuano hiyo inayoendelea nchini Morocco.

Misri, mabingwa mara nyingi zaidi katika historia ya AFCON, walihitaji dakika 120 kujihakikishia ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Benin.

Marwan Attia aliwatanguliza ‘Mafarao’ katika dakika ya 70 lakini Jodel Dossou aliirejesha mchezoni Benin kwa bao lake la dakika ya 83.

Zikiwa zimeongezwa dakika 30, Misri walipata bao la pili kupitia kwa Yasser Ibrahim aliyefunga kwa kichwa.

Katika dakika ya 120, Salah aliimaliza Benin kwa kufunga bao lake la tatu msimu huu wa mashindano hayo ya AFCON.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img